Mipango ya Uchumi na Maendeleo
Idara ya Mipango ya Uchumi na Maendeleo, inaandaa na kusimamia miradi mbali mbali katika jimbo. Lengo ni kupambana dhidi ya uharibifu wa mazingira, kuongeza mapato ya jimbo na kupunguza umasikini wa washirika wa Kikristo wa Moravian. Miongoni mwa miradi ambayo idara inasimamia ni, kwa mfano Shamba Darasa, mradi ambao wakulima wanafundishwa wawe na ufanisi zaidi, mradi wa msitu na mradi wa miparachichi.
Shughuli nyingine ya idara ni kuandaa semina juu ya maendeleo ya kiuchumi kwa idara tofauti na kukuza uwezo wa kujijenga ndani ya kanisa. Ofisi ya idara iko katika Ofisi yetu kuu, Rungwe.
Mawasiliano
Kanisa
la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini
Mipango ya Uchumi na Maendeleo
S.L.P. 32
Tukuyu
Tanzania
Simu: +255 768 458261
Barua Pepe: wamashimbi@yahoo.co.uk