Idara ya Nyaraka na Makumbusho Rungwe

Kanisa la Rungwe ndo la kwanza na lipo hadi hivi leo, Vilevile Makao Makuu ya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini mwa Tanzania bado yapo hapa RAMC Kwenye Jubilei ya miaka 100 ya (KMKT) mwaka 1991, Mradi wa Jumba la Nyaraka na Makumbusho ulianzishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanisa Bwana. Angetile Musomba kwa lengo la Kukusanya, Kuunganisha na Kutunza (Vitu Nyaraka na Picha) za historia ya Kanisa la Moravian Tanzania Nyada za Juu Kusini na watu wanaopatikana Eneo hili.

Mwaka 2011 imejenga Idara ndani ya KMT-JK, na sasa  ikiongozwa na kusimamiwa na Mch. Stephen Mwaipopo. Kwa ajili ya kuunganisha Idara hii na Taasisi nyingine na Jamii, Bodi ya Ushauri ilianzishwa ikikusanya mawazo mbalimbali kumsaidia Mtunza Nyaraka kuandaa na kufanya kazi ndani ya RAMC.
Makumbusho

Katika maonyesho ya makumbusho vitu vinavyoonyeshwa hutueleza kuhusu mambo ya nyanja za maisha ya kimila, mambo ya tiba, ngoma za asili, uwindaji na mitindo ya mavazi, ya watu kutoka maeneo haya, wakiwemo Wanyakyusa na Wandali. Picha za kihistoria za kutoka katika mkusanyiko wa Jumba la Nyaraka na kuhifadhi nyanja mbalimbali za Kitamaduni, na hazioneshi katika uhalisia wake. Nyaraka hizi za thamani hutuonyesha pia jinsi Wamishenari wa Kimoravian na wenyeji walivyoshuhudia na kukabiliana na ulimwengu wa mabadiliko.

Watakaotembelea Maonyesho haya watapatakujua zaidi kuhusu Historia ya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, Tanzania. Pia namna Wamishenari wa kwanza walipowasili Rungwe,kusambaa kwa kazi katika eneo hili, na maendeleo ya Kanisa mpaka hivi Leo.


Nyaraka

Kwenye hifadhi ya Nyaraka kuna Nyaraka muhimu za Kihistoria ambazo zilirekebishwa na kupangwa tena kiusalama zaidi ili zihifadhiwe. Utapata ufumbuzi mkubwa mno kuhusu Wamishenari pale utakaposoma shughuli zao kwenye Nyaraka za Kijerumani, Kidachi, Kiingereza, Kinyakyusa au Kiswahili. Ni safari ya kipekee itakayo kupeleka maeneo mbalimbali kama vile, Historia ya Misheni na Kanisa,Kutawazwa kwa Mchungaji wa kwanza wa Kitanzania 1932, Wafungwa wa Kimishenari wa Kijerumani kama Wafugwa wa Kivita 1940, Jumuiya ya Kimataifa ya Wamishenari baada ya Vita ya Pili ya Dunia, na muunganiko na mageuzi ya Kanisa la Moravian Africa katika kipindi cha kupigania Uhuru mwishoni mwa miaka ya 1960’s.
Kwenye taarifa ya safari halisi, utakutana na Wamishenari wadogo ambao walisafiri toka Ulaya hadi Afrika Mashariki wakizungumza Kinyakyusa kwa msaada wa Kamusi ya Wamishenari wa Mwanzo, Au soma kichwa cha habari na ufungue kwenye maktaba yetu ya vitabu. Kwa msaada zaidi kuhusiana na Utafiti Binafsi au wa Kitaalam, wasiliana na Mtunza Nyaraka

Taarifa hii imetolewa kwenye tovuti ya RAMC. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya chini www.rungwe.org.


Mawasiliano


Idara ya Nyaraka na Makumbusho Rungwe (RAMC)
S.L.P. 32
Tukuyu
Tanzania

Simu:       +255 755 092913
Barua Pepe: mtawasuzana@yahoo.com - Katibu wa Makumbusho
        Archivist.RAMC@gmail.com - Mtunza nyaraka
Web:    www.rungwe.org
Kiswahili