Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Songea Moravian
Chuo cha Moravian cha Mafunzo ya Ufundi Songea kilianzishwa mwaka 2014 na Kanisa la Moravian Tanzania – jimbo la Kusini, kwa msaada wa Daktari Fritz Wolfgang na HMH (Herrenhuter Missionshilfe). Nambari ya hati ya usajili ni VET / RVM / PR / 2014 / C / 057. Chuo cha Songea VTC kinatoa kozi zifuatazo:Kozi za muda mrefu (miaka 2):
- Ufungaji wa umeme wa majumbani
- Ushonaji
- Useremala na uundaji (kati ya miezi 3 na mwaka 1)
- Mafunzo ya kompyuta (kati ya wiki 2 na miezi 6)
- Ufungaji wa umeme wa majumbani (kati ya miezi 3 na mwaka 1)
- Ushonaji (kati ya miezi 3 na mwaka 1)
Kwa sasa, wanafunzi 45 wamejiunga na kozi za muda mdefu chuoni kwetu. Ikiwa una nia ya kujiunga na chuo cha Songea Moravian VTC, unaweza kupakua fomu yetu ya kujiunga hapa:Ikiwa una nia ya kujiunga na moja ya kozi zetu fupi unaweza kuangalia gharama na muda wa kozi hizo katika nyaraka zifuatazo:
Vifaa
Tunatoa vifaa
mbalimbali kwa wanafunzi wetu ili viwasaidie kufikia malengo yao. Kuna chumba
cha kompyuta chenye intaneti, karakana ya ufundi wa umeme wa majumbani, na kozi
za ushonaji, pamoja na karakana ya useremala.
Wafanyakazi
Mkuu | Mratibu
wa Mafunzo |
Gwantwa
John Mwandoloma | Conrad Kayombo |
Lengo
Kuwa na ufanisi na nidhamu, kwa lengo la kuwaendeleza vijana wa Tanzania.Mtazamo
Kuwaelimisha na kuwafunza wanafunzi, ili waweze kushindana katika soko la ajira na kujiajiri.Mawasiliano
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Songea Moravian
S.L.P. 222
Songea
Tanzania
Barua Pepe: songeamoravianvtc@gmail.com
Web: www.songeamoravian-vtc.simplesite.com