Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Namtumbo Moravian

Chuo cha ufundi stadi Namtumbo Moravian VTC kilianzishwa mwaka 2016 na kanisa la Moravian Tanzania –jimbo la kusini kwa msaada wa HMH (Herrnhuter missionshilfe ) Chuo kinapatikana mkoa wa RUVUMA ,Wilaya ya NAMTUMBO karibu na ofisi za Halmashauri ya Wilaya Namtumbo mtaa wa BOMANI. Chuo kinapokea wa jinsia zote na dini zote, pia chuo chetu ni bweni na kutwa.


Chuo kimesajilia veta na nactvet

     Veta : VET/RVM/PR/2018/C/091

     Nactvet : REG/NACTVET/0861P      

Kozi zitolewazo

                                         Kozi ndefu

a.       Ufundi umeme wa majumbani

b.     Ufundi kushona na ubunifu wa mavazi

c.       Ufundi magari

                                             kozi fupi

a.       Kompyuta

b.     Nishati Umeme jua

c.       Ufundi magari

d.     Ufundi kushona

e.       Ufundi umeme wa majumbani

Kwa sasa, wanafunzi 35 wamejiunga na kozi zetu za muda mrefu. Pia, tuna mpango wa kutoa kozi ya ufundi wa magari, kuanzia mwaka 2020. Ukipenda kujiunga na chuo cha Nambumbo VTC, unaweza kupakua fomu yetu ya kujiunga hapa.

Vifaa

Tunatoa vifaa mbalimbali vyenye lengo la kuwahakikishia  wanafunzi wetu mazingira mazuri ya kujifunzia. Chuo kina chumba cha kompyuta chenye kompyuta 9 na karakana yenye mashine za kushonea kwa wanafunzi wa ushonaji. Pia kuna mabweni kwa wavulana na wasichana yenye miundombinu ya kisasa, kila bweni lina nafasi kwa wanafunzi 16. Zaidi ya hayo, karakana ya magari inajengwa, kwa ajili ya kutoa kozi ya ufundi wa magari, ambayo itaanza mwaka 2020.

Wafanyakazi

Hivi sasa, walimu watano na mlinzi mmoja wanafanya kazi katika chuo cha Mafunzo ya Ufundi Namtumbo.


Mkuu wa Chuo                                                                   barnabamulundi166@gmail.com  
Mulundi Barnaba Mulundi  -  +255764194737
Mratibu wa Mafunzo
                                                                   sharifunyoni7@gmail.com
Sharifu Mustafa Nyoni 
-         +255748674349
Mhasibu                                                                     edwingrace634@gmail.com
Grace Brown Erdwin -                  +255622979357


Kauli mbiu yetu

"Ufundi kwa maendeleo ya kweli"
Mawasiliano

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Nambumbo Moravian

S.L.P. 77
Namtumbo - Ruvuma
Tanzania

Simu:     +255 764 194737
Barua Pepe:   namtumbomoravianvtc@gmail.com

Kiswahili