Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Kyela Moravian

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Kyela Moravian kilianzishwa mwezi Februari 2002 na mkuu wake wa kwanza Michael Kajuni na Kanisa la Moravian Tanzania –jimbo la Kusini. Nambari yake ya hati ya usajili ni VET / MBY / PR / 2012 / C / 043. Chuo kilianza na wanafunzi wachache na kozi mbili tu, ushonaji, ufundi seremala na uundaji. Wanafunzi wapatao 110 wanasoma Kyela VTC na tunatoa kozi mbali mbali za muda mdefu na muda mfupi:


Kozi za muda mrefu (miaka 2):
  • Useremala na uundaji
  • Ushonaji
  • Ufungaji wa umeme wa majumbani
  • Ufundi wa magari
Kozi za muda mfupi:
  • Mafunzo ya kompyuta (takriban miezi 2)
  • Udereva (wiki 5)
Mbali na masomo ya lazima, tunafundisha ujasiriamali na ujuzi wa maisha katika kozi zetu zote za muda mrefu. Zaidi ya hayo, wanafunzi wetu hupewa vifaa wakati wa kuhitimu, kama vile mashine ya kushonea kwa wanafunzi wa ushonaji. Hii inawawezesha kuanzisha biashara zao na kujitegemea kiuchumi.

Vifaa

Tunatoa vifaa mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wetu. Miongoni mwa vifaa hivyo ni maabara ya kompyuta yenye kompyuta zipatazo 22, madarasa mawili yenye vifaa vya ushonaji, karakana mbili kwa ajili ya wanafunzi wa useremala, na karakana ya ufundi wa magari. Pia tuna bweni kwa wasichana, ambalo linawawezesha kukaa chuoni. Bweni lina nafasi kwa wanafunzi 36.

Wafanyakazi

Kwa sasa tumeajiri walimu saba wa muda mrefu na walimu wawili wa muda mfupi. Kwa kuongezea, tuna wafanyakazi wengine wasaidizi.

MkuuMhasibuMtaaluma mkuu
Michael Kajuni-  +255 764 103046 Happy Kalinga - +255764 476666
Christopher Selemani -  +255764 476666

Mawasiliano

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Kyela Moravian

S.L.P. 36
Kyela-Mbeya
Tanzania

Simu:     +255 764 103046
Barua Pepe:   kyelamoravianvtc@gmail.com
Kiswahili