Shamba la Maparachichi

Shamba la maparachichi la Moravian liko  Rungwe Misheni katika Kijiji cha Ilolo, kata ya Kiwira, wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Mradi ulioanza 2010 una hekta 43.7 na miparachichi 26220. Mradi hutoa kazi kwa wafanyakazi 250. Kwa mwaka 2018, tulivuna maparachichi zaidi ya tani 175.

Tunauza matunda yetu kwa Kampuni ya KUZA Africa, ambayo hupeleka matunda Ufaransa. Zaidi ya hayo, tuna soko la ndani ambapo tunauza matunda katika mifuko ya kilogramu 100 kwa shilingi 65,000-70,000

Kama shirika la kidini tumeamua kuwekeza katika kilimo, hasa uzalishaji wa maparachichi kwa madhumuni yafuatayo.

  1. Kutoa ajira kwa wanawake na vijana wa Taifa hili.
  2. Kuchangia mapato ya kanisa kama shirika linalowasaidia watu kiroho, kijamii na kiuchumi
  3. Kuchangia mapato ya Taifa ya serikali kwa kulipa kodi
  4. Uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti ili kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa kama athari ya kimazingira
  5. Kuchangia serikali katika viwanda katika nchi yenye uchumi wa kati kama sera ya Kitaifa inavyosisitiza.
  6. Kutoa wazo kwa jamii la kupanda miparachichi kama njia nyingine ya kupata kipato.
  7. Kuboresha chakula na afya ya jamii katika kijiji cha Rungwe kwa kula maparachichi yenye lishe.
  8. Kuboresha miundombinu kama mitandao ya simu, mawasiliano na barabara.
Mawasiliano

Robert Clows
+255 784 969580
Kiswahili