Njiwa Media


Njiwa Media ni Mwamvuli ulio chini ya Idara ya habari unaosimamia vyombo vyote vya habari vya Kanisa pamoja mitandao yake ya kijamii. Njiwa Media ilianzishwa baada ya Idara ya habari kuanza rasmi mwanzoni mwa mwaka 2022 ili kufikia maono ya Kanisa kuwa na vyombo vyake vya habari pamoja na Mitandao yake ya jamii. Tayari jina Njiwa Media limesajiliwa na linatambulika katika orodha ya majina ya biashara chini ya msajili wa makampuni Brela.


MAJUKUMU YA NJIWA MEDIA.

1.       Kuhabarisha

2.       Kusambaza Injili

3.       Kunadi miradi ya kanisa

4.       Kuinua na kukuza vipawa ndani ya Kanisa.

MAFANIKIO YA NJIWA MEDIA.

Tangu kuanzishwa kwake, Njiwa Media imepata mafanikio kadhaa kama ifuatavyo.

1.       Imefanikiwa kuifikia jamii kubwa kupitia mitandao yao ya kijamii

2.       Imefanikiwa kuinadi baadhi ya miradi ya kanisa

3.       Imefanikiwa kupata heshima ya kuchukua Tuzo ya chombo cha habari bora katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

4.       Imefanikiwa kulitangaza Kanisa la Moravian na nembo yake ya mwana kondoo

TUTEMBELEE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
NJIWA ONLINE TV {YOU TUBE}
MSIMAMIZI MKUU WA NJIWA MEDIA
Gwamaka Jongo
S.L.P 32
Tukuyu
+255761325346
jongogwamaka@gmail.com
Kiswahili