Nyumba ya Wageni Mbutusyo

Nyumba ya Wageni Mbutusyo

Nyumba ya Wageni ya Mbutusyo ilianzishwa na Idara ya Ustawi wa Jamii ya Kanisa la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini. Ni jengo zuri la muda mrefu, lililokarabatiwa mwaka 2017 tangu wakati huo ni mojawapo ya mahali bora zaidi pa kukaa wilayani Rungwe. Eneo tulivu lililoizunguka nyumba ya wageni na umuhimu wa historia ya mkoa vitakupatia maarifa ya kipekee.

Kanisa la kwanza kabisa lililojengwa na Wamisionari wa Kanisa la Moravian nchini Tanzania lipo mita chache tu kutoka nyumba ya wageni. Kwa watu wanaovutiwa na historia ya wamisionari na wilaya ya Rungwe, kuna jengo la Nyaraka na Makumbusho Rungwe, karibu kabisa na nyumba ya wageni Mbutusyo.

Huduma ya malazi

  • Chumba cha kitanda kimoja (single bedroom) - Tsh. 50,000  kwa usiku
  • Chumba cha vitanda viwili (double bedroom) - Tsh. 60,000 kwa usiku
  • Chumba cha vitanda viwili (twin bedroom) - Tsh. 60,000 kwa usiku

Pia, tunatoza shilingi 20,000 kwa siku kwa ajili ya malipo ya Mhudumu anayefanya usafi. Hata hivyo, kiasi hicho kinagawanywa kati ya wageni wote wanaoishi katika nyumba ya wageni ya Mbutusyo.


Bei ya chakula
  • Chakula cha asubuhi  Tsh. 5,000 
  • Chakula cha mchana  Tsh. 15,000 
  • Chakula cha jioni  Tsh. 15,000

Milo yetu inatayarishwa kwa kutumia bidhaa za ndani, tunaweza kuandaa chakula chochote kulingana na upendeleo wa mteja.


Chumba chetu cha chakula
Eneo la nje la kupumzika

Mawasiliano

Nyumba ya Wageni Mbutusyo

S.L.P. 32
Tukuyu
Mbeya Region
Tanzania

Barua Pepe:  butusyoguest@gmail.com
         liliemanuel@gmail.com

                              butusyoguest@gmail.com


Simu:        +255 764 934339
        +255 748 104700

Kiswahili