Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Nambumbo Moravian
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Namtumbo kilianzishwa mwaka 2016 na Kanisa la Moravian Tanzania – jimbo la Kusini, kwa msaada wa HMH (Herrnhuter Missionshilfe). Tunakaribisha wanafunzi wa aina zote bila kujali utofauti wa kiuchumi na wa kidini, lengo kuleta maendeleo katika jamii.Tunatoa kozi zifuatazo:
Kozi za muda mrefu (miaka 2):
- Ufundi wa umeme wa majumbani
- Ushonaji
Kozi za muda mfupi (miezi 3 hadi mwaka 1)
- Ufundi wa umeme wa majumbani
- Ushonaji
- Mafunzo ya kompyuta
Nambari ya hati ya usajili wa chuo ni VET / RVM / PR / 2018 / C / 091.
Vifaa
Tunatoa vifaa mbalimbali vyenye lengo la kuwahakikishia wanafunzi wetu mazingira mazuri ya kujifunzia. Chuo kina chumba cha kompyuta chenye kompyuta 9 na karakana yenye mashine za kushonea kwa wanafunzi wa ushonaji. Pia kuna mabweni kwa wavulana na wasichana yenye miundombinu ya kisasa, kila bweni lina nafasi kwa wanafunzi 16. Zaidi ya hayo, karakana ya magari inajengwa, kwa ajili ya kutoa kozi ya ufundi wa magari, ambayo itaanza mwaka 2020.Wafanyakazi
Hivi sasa, walimu watano na mlinzi mmoja wanafanya kazi katika chuo cha Mafunzo ya Ufundi Namtumbo.Mkuu | Makamu Mkuu |
Barnaba
Mulundi | Gibson Mwamahonje |
Kauli mbiu ya Shule
Kama unaona ufundi ni ujinga, jaribua kuwa mjinga.
"If you are being told that vocational training education is ignorant, try to be ignorant."
Mawasiliano
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Nambumbo Moravian
S.L.P. 77
Namtumbo - Ruvuma
Tanzania
Simu: +255 764
194737
Barua Pepe: namtumbomoravianvtc@gmail.com